News

Yanga na kufuzu nusu fainali ya kombe la shirikisho barani Africa.

Download, Listen, and Share.

Yanga imekuwa ikiendelea na mazoezi yao yanayofanyika jioni pale Avic Town na kama unataka kujua kipi kinapikwa huko basi tambua makocha wa timu hiyo wamekomaa na idara mbili kubwa za ulinzi na ile ya ushambuliaji.

Kocha wa Yanga Nasreddine Nabi na msaidizi wake Cedric Kaze wamekuwa wakali kwenye mchezo huu kwa kuwa wameona kama wachezaji wanaweza kubweteka kutokana na matokeo ya mchezo wa kwanza nchini Nigeria.

Hata hivyo mbali na mengine yote yanga amekuwa na historia nzuri ya ushindi kwenye uwanja wake wa nyumbani hivyo kupelekea mechi hiyo kuwa upande wao zaidi kutokana na matokeo yote ya michezo aliocheza hapa nyumbani.

Kesho mchezo wao huo unatarajia kuchezwa muda wa saa moja kamili usiku kwa mtazamo wa washabiki wengi yanga ananafasi kubwa ya kushinda katika mchezo huo kutokana na motisha walizokuwa nazo kuanzia viongozi mpaka mashabiki wao ka ngazi zote.

About the author

Jackie's Empire