News

WCB waondoka na tuzo 8 TMA, Zuchu kinara wa tuzo aondokaa na tuzo 5

Download, Listen, and Share.

Malkia wa Muziki wa BongoFleva kutoka Label ya @wcb_wasafi @officialzuchu ameng’ara kwa kushinda Tuzo nyingi zaidi katika Tuzo za Muziki Tanzania TMA2022 zilizotolewa Usiku wa kuamkia leo.

Rais wa lebo hiyo Diamond ameusika katika tuzo mbili, Msanii wa Kiume chaguo la mtandao pamoja na kolabo bora akiwa na RayVanny.

Mbosso ameshinda tuzo ya msanii bora wa kiume na kufanya WCB kuondoka na tuzo 8.

1. Msanii Bora Wa Kike Wa Mwaka
2. Video Bora Ya Mwaka (Mwambieni)
3. Mwimbaji Bora Wa Kike Wa Bongofleva
4. Wimbo Bora Wa Bongofleva (Kwikwi)
5. Mwanamuziki Bora Wa Kike Chaguo La Watu Kidigitali

Haikuwa rahisi jitihada na nguvu kubwa imetumika katika kufanikisha hili uwekezaji wenye tija unaogfanywa na raisi wa WCB ndio chachu ya mafanikio haya hawakupanda tuu , akili na maarifa yanatumika katika kuendesha shughuli zao hizo za muziki nchini tanzania na nje ya hapa.

About the author

Jackie's Empire